Thursday, December 11, 2025
spot_img
HomeHabariMasheikh waunga mkono hatua za Rais Samia kurejesha amani baada ya vurugu

Masheikh waunga mkono hatua za Rais Samia kurejesha amani baada ya vurugu

Taasisi za Kiislamu na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), zimeunga mkono hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya vurugu za Oktoba 29, ikiwemo kuunda tume ya uchunguzi wa uvunjifu wa amani.

Hatua nyingine iliyoungwa mkono na taasisi hizo, ni mchakato wa maridhiano, huku zikisisitiza zitashiriki na kutoa mchango wao katika mchakato huo.

Uungaji mkono huo ni sehemu ya maazimio ya taasisi hizo baada ya kutafakari kwa kina kuhusu yaliyotokea Oktoba 29 na 30, mwaka huu.

Azimio hilo, limetolewa, Novemba 20, 2025 na Amiri wa Baraza Kuu na Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha katika Msikiti wa Mohammed VI, Dar es Salaam.

“Tunaunga mkono hatua ya Rais Samia kuunda Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjivu wa amani yaliyotokea Oktoba 29.

“Pia tuko tayari kuwa daraja la kuunganisha Watanzania, tunapendekeza uwepo uchunguzi wa kina, usiopendelea upande wowote, ili kubaini watu waliochochea, waliopanga na kuratibu uhalifu uliotokea,” ameeleza Sheikh Kundecha.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments