Mashujaa kuongeza wachezaji wanne dirisha dogo

Uongozi wa Klabu ya Mashujaa umetangaza mpango wa kusajili wachezaji wanne wakati wa dirisha dogo la usajili ili kuimarisha kikosi chao kwa msimu huu.

Meneja wa timu hiyo, Athumani Amiri, amesema maboresho yatakuwa kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi kwa lengo la kuongeza ushindani na kufikia malengo ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.

“Tunahitaji wachezaji wenye viwango vya juu bila kujali ukubwa wa majina yao. Tunaendelea na mazungumzo na wachezaji tunaowahitaji,” alisema Amiri.

Kwa sasa kikosi cha Mashujaa kinaendelea na maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaochezwa Desemba 28. Timu inatarajia kuelekea Dodoma mapema ili wachezaji wazoeane na hali ya hewa tofauti na Kigoma.

Ligi Kuu Tanzania Bara inaongozwa na Simba SC yenye pointi 34, huku KenGold ikiwa nafasi ya mwisho kwa pointi sita.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *