Mashujaa yachukua kitasa Pamba

Mashujaa FC imemsajili beki wa kati wa Pamba Jiji, Samson Madeleke, akichukua nafasi ya Ame Ibrahim aliyejiunga na Mbeya City.

Madeleke, ambaye aliwahi pia kucheza Mbeya City na Mashujaa, anakuwa mchezaji wa 11 kusajiliwa na klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

Mashujaa tayari imesajili wachezaji kadhaa akiwemo Selemani Bwenzi (KenGold), Omari Omari (Simba – mkopo), na Ismail Mgunda (AS Vita).

Timu hiyo ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya saba na pointi 35 na tayari imeanza mazoezi jijini Dar es Salaam kabla ya kambi rasmi Kigoma.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *