Matukio mbalimbali yamejiri katika mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na makundi mbalimbali ya walinzi wa jadi (Sungusungu), uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, mkoani Mwanza, tarehe 20 Juni, 2025.

Mkutano huo umehudhuriwa na maelfu ya wananchi pamoja na makundi ya walinzi wa jadi kutoka maeneo mbalimbali nchini, ukiwa na lengo la kuimarisha mahusiano kati ya serikali na walinzi wa jadi katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
Katika mkutano huo, Rais Samia aliwapongeza walinzi wa jadi kwa mchango wao katika ulinzi wa jamii na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya dola ili kuhakikisha usalama unadumishwa kwa mujibu wa sheria.







