Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amesema haoni shida kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ili kupata watendaji sahihi watakaotekeleza majukumu yao kwa moyo mmoja.
Ameeleza hayo Novemba 18,2025 katika uapisho wa mawaziri na manaibu mawaziri waliopishwa Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.
“Sioni kubadilisha mnanjiua kipindi fulani mlishanisema nabadalisha sana, nikasema ndio nabadilisha hadi nipate yule atakayefanya kazi sana na mimi kwa moyo mmoja,”
Dk Samia amewaambia mawaziri hao kuwa kazi ya kubwa kuwajibika kwa wananchi na Taifa, akisema mambo yaliyoahidiwa kwa Watanzania ni mengi, kama alivyogusia akizundua Bunge hivi karibuni.
“Mambo tuliaahidi ni mengi muda wa kuyatekeleza ni mchache sana, kwa wale mlioapa leo aliyekuwa mzito akipunguze kilo kidogo,”
“Tuna kazi ya kwenda mbio, muda ni mchache na mambo mengine mnoo…,” ameeleza.




