Maximo aanza kazi – KMC kuikabili KMKM Zanzibar

KMC itacheza mechi ya kirafiki Jumapili dhidi ya KMKM ya Zanzibar ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya chini ya Kocha Marcio Maximo.

Msemaji wa KMC, Khalid Chukuchuku, alisema mchezo huo utampa Maximo nafasi ya kuwapima wachezaji wote, huku kikosi kikiwa bila majeruhi.

KMC inalenga kumaliza nafasi za juu kwenye Ligi Kuu na imewataka mashabiki wa Kinondoni kuendelea kuiunga mkono timu hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *