TAIFA la Tanzania bado lipo kwenye mikono salama usiku huu baada ya Bondia Mtanzania Mchanja Yohana kutembeza kichapo usiku huu kwa kumchapa makonde ya kutosha Bondia kutoka Philipino Miel Fajardo na kushinda kwa pointi 116 kwa 111 za majaji wote watatu kwenye pambano la Raundi 12 kwenye pambano la #KnockOutYaMama ndani ya ukumbi wa Super Dome hapa Masaki usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kushinda mkanda wa World Boxing Organization Global flyweight championship (WBO Global).

Kwa ushindi huo wa pointi, Mchanja anaondoka na kitita cha #KnockoutYaMama cha Shilingi Milioni tano (5 Milioni).
KnockoutYaMama



