
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Tawi la CCM Kijiji cha Mihima Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Saidi Mbila na wanachama wengine 250 wa chama hicho wamejiunga ACT Wazalendo.
Miongoni mwao wapo mshindi wa pili na watatu wa kura za maoni za CCM. Wanachama hao walipokelewa jana Oktoba 29, 2024 na Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita.
Aliyeshika nafasi ya tatu katika kura za maoni za CCM, Yunus Nurdin Leonard ndiye aliyeanzisha vuguvugu la kukihama chama hicho kufuatia madai ya ubadhilifu wa mali za umma na wizi uliokithiri kwenye zoezi la kumpata mpeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mtaa.
“Nilipokuwa Mwenezi wa UVCCM Tawi nilihoji matumizi ya Shilingi milioni 217 za mauzo ya mazao ya misitu, lakini nikaishia kubambikiwa kesi, sasa nimekuja kugombea wakaiba na kuweka mtu wao. Sasa mimi na wenzangu tumeamua kujiunga ACT Wazalendo.” alisema Yunus Leonard.

Wakati akiwapokea wanachama hao kutoka CCM, Mchinjita alisema, “Nina wakaribisha,. ACT Wazalendo ndicho chama chenye sera mbadala. Sera zenye majawabu yote ya changamoto na matatizo yanayomkabili Mwananchi.” alisemaÂ
Katika hatua nyingine,Mchinjita aliitaka TAKUKURU ichunguze tuhuma za ubadhilifu wa mali ya umma zilizoibuliwa na Yunus Nurdin. Aidha alitoa agizo kwa Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo aandike barua rasmi kuomba jambo hilo lichunguzwe na vyombo vya dola.
Aidha Yunusi Nurdin Leonard ameshachukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa Kijiji cha Mihima kwa kupitia Chama cha ACT Wazalendo.

