Saturday, November 1, 2025
spot_img
HomeElimuMdhibiti ubora ataka wazazi kuzingatia shule bora

Mdhibiti ubora ataka wazazi kuzingatia shule bora

Afisa Mdhibiti Mkuu Ubora wa Shule Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Asha Kiliza, amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanaohitimu elimu ya awali wanaandikishwa mapema kuanza masomo ya darasa la kwanza kwa mwaka wa masomo 2026.

Amesema wazazi wanaowapeleka watoto wao shule binafsi wanatakiwa kuzingatia zile shule ambazo zimesajiliwa na kufuata mtaala ulioboreahwa, ili kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango rasmi.

Asha amesema hayo Oktoba 16, 2025, aliposhiriki mahafali ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya awali katika Shule ya Msingi The Finest, iliyopo Kibaha.

Aidha, amefafanua kuwa ofisi yake imekuwa ikitoa semina za elekezi kwa shule binafsi juu ya mtaala ulioboreahwa, na kushirikiana na wakaguzi kukagua shule hizo kabla hazijapokea wanafunzi. Semina hizo zimejikita katika nyanja nane zikiwemo: mtaala unaotumika, vifaa vya mtaala, mazingira ya shule, na maadili ya wanafunzi.

Awali, Mkurugenzi wa shule hiyo, Abubakar Alawi, amesema shule ilianzishwa Oktoba 2023 ikiwa na wanafunzi wawili na mwalimu mmoja, lakini sasa imefikia wanafunzi 362 na walimu 15.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Pro. Mrisho Malipula, amewataka wazazi kutoa ushirikiano endelevu kwa kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na kulipa ada kwa wakati ili kuepusha mipango ya shule kukwama.

Ameiomba pia Serikali kuboresha miundombinu ya barabara eneo hilo ili kuondoa changamoto za magari kuharibika na baadhi ya maeneo kutopitika kipindi cha mvua.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments