Sunday, March 29, 2026
spot_img
HomeMichezoMendy aishambulia CAF vikali kuhusu maamuzi AFCON 2025

Mendy aishambulia CAF vikali kuhusu maamuzi AFCON 2025

Kipa wa kimataifa wa Senegal, Édouard Mendy, ameibuka na kauli kali dhidi ya Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF, kufuatia maamuzi yaliyofanyika katika michuano ya AFCON 2025.

Mendy amesema kuwa hashangazwi na maamuzi hayo, akidai kuwa CAF ni taasisi ambayo haikui kwa kasi sawa na maendeleo ya soka la Afrika. Amesisitiza kuwa licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na wachezaji pamoja na wadau wa soka barani Afrika kuinua kiwango cha mchezo huo duniani, bado kuna changamoto kubwa katika uongozi wa juu wa taasisi hiyo.

‎“Watu wanaohusika katika soka la Afrika wanafanya kazi kubwa kila siku duniani kote kuhakikisha soka la Afrika linafika kiwango cha juu zaidi. Lakini kwa bahati mbaya, kuna kundi dogo la watu linaamua hatma ya mchezo wetu, na siyo watu sahihi kwa majukumu hayo,” alisema Mendy.

‎Kipa huyo wa Senegal national team ameongeza kuwa matatizo hayo si ya sasa pekee, bali yamekuwepo kwa muda mrefu, huku AFCON ya mwaka 2025 ikiwa ni kilele cha malalamiko hayo.

‎Aidha, Mendy ameitaka CAF kufanya tathmini ya kina ya mfumo wake wa uendeshaji, akisisitiza kuwa mabadiliko makubwa yanahitajika haraka ili kuboresha taswira ya soka la Afrika kimataifa.

‎“Ni wazi kuwa katika wiki au miezi ijayo, taasisi hii italazimika kujitathmini upya na kufanya mageuzi makubwa. Kwa sasa, kuna mapungufu makubwa katika uendeshaji wake ambayo yanatunyima nafasi ya kuonekana vizuri kimataifa,” aliongeza.

Kauli ya Mendy imezua mjadala mpana miongoni mwa wadau wa soka barani Afrika, wengi wakitaka kuona mabadiliko ya kweli ndani ya CAF ili kuendana na kasi ya maendeleo ya soka la kisasa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments