Klabu ya Pamba Jiji imemsajili rasmi mfungaji bora wa Ligi Kuu Zanzibar 2024/2025, Abdallah Idd Pina, kutoka Mlandege FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Pina alifunga mabao 21 na kutoa pasi 12 msimu uliopita.
Pia, imempokea kiungo mkabaji Kelvin Nashon kwa mkopo kutoka Singida Black Stars ili kumpa muda zaidi wa kucheza.
Pamba Jiji tayari imeanza maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza Septemba 16.


