Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariMgombea ubunge ataja atachofanyasiku 100 akiwa madarakani

Mgombea ubunge ataja atachofanyasiku 100 akiwa madarakani

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHAUMMA), Moza Ally amesema moja ya mikakati yake endapo atashinda nafasi hiyo ni kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inawafikia walengwa.

Amesema atatekeleza ahadi hiyo ndani ya siku 100 tu toka atakapotangazwa kushinda nafasi hiyo.

Alitoa ahadi hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika mkutano wa wa kampeni, uliofanyika Uwanja wa Sumaye, Kata ya Kigogo wilayani Kinondoni.

Alisema ndani ya siku atasimamia kuhakikisha wanawake, wenye ulemavu na vijana wameunda vikundi kwa usawa bila upendeleo na wanapata mikopo kwa njia stahiki.

Alisema: “kwa kuwa Nitakuwa mwakilishi wa wananchi wa Kinondoni, sitaruhusu mikopo hiyo itolewe kwa upendeleo, vikundi vitakavyoundwa vitakuwa halisi na vya wazi”.

Alisema ili kufanikisha hilo atapita nyumba kwa nyumba kuandikisha majina ya wananchi wenye nia ya kupata mikopo.

Moza alisema dani ya siku hizo katika ofisi yake atakuwepo mwanasheria ambaye jukumu lake ni kutoa usaidizi wa kisheria kwa vikundi vyote ili vikidhi uhalali wa kukopeshwa.

Alisema wananchi hawatalazimika kuandaa fedha ili kuingia ofisini kwake na kumwona, bali watapata fursa hiyo kila pale watakapohitaji.

“Nitakuwa Mbunge wa watu, sitokuwa mbunge wa mfukoni. Nitahakikisha nawatumikia wananchi wa Jimbo la Kinondoni wakiwemo wa Kata ya Kigogo. Nipeni imani yenu,” alisema Moza.

Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo aliwataka wananchi wa Kinondoni kuhakikisha Oktoba 29, wanakwenda kupiga kura kwa wagombea wa chama hicho.

Alisema chama hicho kina dira inayolenga kutoa lishe bora kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuwajenga kiakili.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments