Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Haran Sanga, ameendelea na kampeni zake ambapo alikutana na wananchi wa Kata ya Vijibweni, Jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wa kampeni, Sanga amewahakikishia wakazi wa Kigamboni kuwa ataweka kipaumbele katika kushughulikia changamoto zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, huduma bora za afya pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.



Amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia, changamoto hizo ambazo zimekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi wa Kigamboni zitakuwa historia, na maisha ya wananchi yataboreka kwa kiwango kikubwa.




