Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, akiambatana na Mgombea Mwenza wake Fatma Fereji, jana Agosti 25, 2025, walifika katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria zinazohusu uchaguzi mkuu.

Katika hatua hiyo, wagombea hao walikula kiapo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Hussein Mtembwa, ikiwa ni miongoni mwa masharti ya kisheria yanayowataka wagombea wote wa nafasi ya urais kutimiza sharti hilo kabla ya kuanza rasmi kampeni.










