Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomeHabariMkakati wa Maji Bomang’ombe Waendelea, Tanki Jipya Lakamilika

Mkakati wa Maji Bomang’ombe Waendelea, Tanki Jipya Lakamilika

Mbunge wa Jimbo la Hai, Mafue Sahasisha, amesema mkakati wa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la maji katika Mji wa Bomang’ombe na viunga vyake unaendelea kuzaa matunda baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki jipya la maji kutoka chanzo cha Kikafu.

Amesema kwa sasa hatua inayoendelea ni zoezi la kuvusha mipira chini ya barabara kuelekea kwenye tanki kubwa la Sadala, hatua ambayo itawezesha maji kuingizwa kwenye tanki hilo na kuanza kusambazwa kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, kukamilika kwa hatua hiyo kutaboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Bomang’ombe na maeneo ya jirani, huku akisisitiza kuwa juhudi zinaendelea ili kuhakikisha changamoto ya maji inakuwa historia kwa wananchi wa Jimbo la Hai.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments