Mlandege SC, wawakilishi wa Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wametangaza kuachana na wachezaji watano akiwemo Ally Mohamed Njiwa na Benson Young.

Mmiliki wa timu, Abdulsatar Daud, amesema wameamua kuachana nao kutokana na kushuka kwa viwango na mpango wa kuunda kikosi chenye ushindani kwa msimu wa 2025/26, wakianzia kwenye michuano ya kimataifa.


