Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, Mlandege FC, wanaendelea kukosea mwelekeo baada ya kupata sare ya tano katika mechi nane walizocheza, safari hii wakitoka 1-1 dhidi ya Zimamoto FC.
Mlandege imekusanya alama 11, ikiwa nafasi ya saba, ikishinda mechi mbili tu na kupoteza moja. Kocha Msaidizi Sabri China amesema timu haijapoteza ubora bali inakosa bahati ya kupata alama tatu, akisisitiza viwango vimeongezeka kutokana na upinzani mkubwa wa ligi.
China amesema maboresho kidogo ya umakini kwa washambuliaji yanahitajika na kuwaomba mashabiki waendelee kuwa wavumilivu wakati kikosi kikikamilisha kipindi hiki cha mpito.




