MNH kuunda kambi tatizo la maumivu ya viungo

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa kushirikiana na taasisi ya ROAD2IR ya nchini Marekani, watafanya kambi maalum ya uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa wenye maumivu makali ya viungo ikiwamo wanaougua saratani.

Kambi hiyo Bingwa Mbobezi wa matibabu hayo duniani, Prof. David Prologo kutoka Emory Health Care ya Marekani, ikilenga kuuchunguza mwili sehemu mbalimbali, kwa njia ya kisasa ya tiba radiolojia.

Tiba radiolojia ni aina ya taaluma ya matibabu ambayo daktari bingwa mbobezi hutumia teknolojia ya picha za uchunguzi za (Angio-Suite, CT, Xray, Ultrasound), kumuongoza kufanya uchunguzi au tiba kupitia matundu madogo mwilini bila kufanya upasuaji.

Bingwa Mbobezi wa Tiba Radiolojia MNH, Dk. Erick Mbuguje, alisema kambi hii itahusisha matibabu ya wagonjwa wenye maumivu makali ya aina zote yaliyogawanyika katika makundi makuu mawili, maumivu ya mgongo na maumivu ya sehemu nyingine za mwili.

Alifafanua kuwa katika kundi la kwanza ni wagonjwa wenye maumivu makali ya mgongo yasiyosababishwa na saratani ni pamoja na pingili zilizosagika, kuvunjika au kupukutika na matibabu ya maumivu hayo hayahusishi upasuaji.

Chanzo: Nipashe

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *