Kocha raia wa Afrika Kusini, Rulani Mokwena, juzi alitangaza rasmi kuachana na klabu ya MC Alger inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria.
Kwa mujibu wa duru za michezo barani Afrika, Mokwena anatajwa kuwa katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Al Ittihad inayoshiriki ligi kuu ya Libya.
Wakati huo huo, kocha Khaled Ben Yahia naye ameondoka katika klabu ya Al Ittihad, akitarajiwa kurejea MC Alger kuchukua nafasi iliyoachwa wazi.
Mabadiliko haya yameibua gumzo kubwa miongoni mwa wadau wa soka, hasa kutokana na hali ya makocha hao kubadilishana vilabu. Kabla ya kujiunga na Al Ittihad, Ben Yahia alikuwa Kocha Mkuu wa MC Alger, huku Mokwena akielekea Al Ittihad akitokea MC Alger—hali inayofanana na kubadilishana nafasi kati yao.




