Morocco: “Kazi ndio inaanza”

📌Baada ya Taifa Stars kutinga Robo Fainali CHAN 2024

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman “Morocco”, amesema safari yao kwenye CHAN 2024 ndio inaanza licha ya kufuzu robo fainali wakiwa na pointi tisa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Jamhuri ya Kati.

Amesema hatua za juu ndizo zenye ugumu zaidi hivyo watalazimika kupambana mara mbili. Stars imeifunga Burkina Faso 2-0, Mauritania 1-0 na Madagascar 2-1, na inatarajia kuendeleza rekodi hiyo kabla ya hatua inayofuata.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *