MSD yapata tuzo kwa kuwezesha matibabu ya moyo nchini

Bohari ya Dawa (MSD) imetunukiwa tuzo maalum na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kutambua mchango na ushirikiano wake katika kuboresha huduma na matibabu ya Programu za Moyo nchini.

Tuzo hiyo maalum, ilikabidhiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Nassor Ahmed Mazrui, wakati akifunga mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo, ulioandaliwa na taasisi ya JKCI na kufanyika kwa siku tatu, visiwani humo.

MSD imekuwa mshirika muhimu wa JKCI katika kuboresha huduma za programu za Moyo nchini, kwa kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa uhakika wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya moyo nchini.

MSD imehakikisha inaisambaza Dawa na Vifaa tiba vya kisasa kwa JKCI, ikiwemo mashine zenye teknlojia ya Akili Mnemba (AI), hatua ambayo imesaidia kuboresha afya za watanzania wenye changamoto za Magonjwa ya Moyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *