MSD yatunukiwa tuzo ya umahiri wa utoaji huduma

Bohari ya Dawa (MSD) imetunukiwa Tuzo ya Umahiri wa Utoaji Huduma katika Sekta ya Famasi nchini (Award of Service Excellence in Pharmaceutical Sector) kupitia Tuzo za Tanzania Service Excellence Award 2024, zilizoandaliwa na Taasisi ya Charted Institute of Customer Service (CICM).

Tuzo hizo zilitolewa jana katika hafla maalum iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Holiday Inn, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Gendi Machumani, alisema kuwa kutunukiwa tuzo ya utoaji huduma bora katika sekta ya afya ni ishara ya kuthaminiwa kwa huduma bora zinazotolewa na MSD.

Gendi alisisitiza kuwa tuzo hiyo inadhihirisha mabadiliko makubwa ya kitaasisi chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu, Mavere Tukai, ambapo MSD imefanikiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kufanikisha malengo yake ya kuboresha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.

Aidha, aliongeza kuwa tuzo hiyo inawapa msukumo zaidi wa kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya zenye ubora, gharama nafuu, na kwa wakati muafaka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *