Mshindi wa Tap Kibingwa aondoka na Suzuki Fronx mpya

Benki ya Stanbic na Visa wahitimisha kampeni hiyo nchi nzima kwa makabidhiano ya zawadi kuu jijini Dar es Salaam

Edwin Shayo anyakua gari ya kifahari  Suzuki Fronx baada ya miezi mitatu ya zawadi za kidijitali

• Zaidi ya asilimia 80% ya wateja wanaohusika, TZS 7.5 milioni zilizotolewa kama zawadi ya fedha taslimu, na matumizi ya kadi za kidijitali kupanda kwa asilimia 20%.

Benki ya Stanbic Tanzania, kwa kushirikiana na Visa, leo wamekamilisha fainali yake ya Kampeni ya Tap Kibingwa kwa   mafanikio makubwa kwa kumkabidhi rasmi mshindi wa zawadi kuu ya Suzuki Fronx, Edwin Shayo.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika eneo la kazi la mshindi huyo Mikocheni, huku ukiongozwa na msafara uliopambwa na chapa ya Stanbic kutoka makao makuu—wakisherehekea sio tu kwa kupata mshindi bali mabadiliko makubwa katika jinsi Watanzania wanavyojihusisha na benki  kidijitali.

Kampeni ya Tap Kibingwa ilianza Januari hadi Aprili 2025, ikiwa na dhamira ya wazi: kutumia miamala bila pesa taslimu na kuzawadia wateja ambao walitumia kikamilifu Kadi zao za Debit za Visa kwa malipo ya kila siku. Kupitia mpango huu, Benki ya Stanbic iliimarisha jukumu lake kama kichocheo cha ujumuishaji wa kifedha, uvumbuzi wa malipo, na suluhisho za kibenki zinazozingatia wateja.

“Tap Kibingwa ilikuwa zaidi ya kampeni-ilikuwa harakati ya kuwasaidia Watanzania kupata urahisi na usalama wa malipo ya kidijitali,” alisema Shangwe Kisanji, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya Stanbic Tanzania. “Leo tunasherehekea sio tu ushindi wa Edwin lakini maelfu ya wateja waliochagua kutumia huduma ya kidijitali mara kwa mara na bila kusita.”

Katika muda wote wa kampeni, Stanbic ilitoa droo tatu za kila mwezi, kila moja ikiwazawadia wateja watano TZS 500,000. Kwa jumla, wateja 15 walipata TZS 7.5 milioni kama zawadi ya fedha taslimu. Matarajio yaliongezeka, huku zaidi ya asilimia 80% ya wateja wakishiriki na ongezeko la asilimia 20% la matumizi ya Visa Debit Card kwa wateja wa Stanbic.

Kivutio kikuu cha kampeni hiyo kilikuwa ni makabidhiano  ya Suzuki Fronx ya mwaka 2024 yenye matumizi ya umbali usiozidi maili sifuri, alizawadiwa Edwin Shayo kwa kushinda katika droo kuu kupitia matumizi yake ya mara kwa mara ya kadi ya thamani ya juu.

“Kushinda gari hili ni baraka, na ninaishukuru Stanbic kwa mpango huu wa kipekee,” alisema Edwin Shayo. “Zaidi ya kila kitu kwa  sasa naona umuhimu wa kutokuwa na pesa taslimu. Ni matumizi ya Visa ambayo ni ya haraka, salama, na rahisi zaidi.”

Kampeni hii inawiana kwa karibu na agizo la Benki Kuu la Tanzania la kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha za kidijitali na kupunguza utegemezi wa fedha taslimu, hasa wakati taifa linavyozidi kushika kasi kuelekea uchumi shirikishi na unaoendeshwa na teknolojia.

“Kampeni hii inaunga mkono moja kwa moja malengo ya sekta ya fedha ya Tanzania,” aliongeza Shangwe. “Katika Stanbic, tunajivunia kuongoza mabadiliko haya. Tunaamini kufanya zaidi ya benki katika kuleta athari chanya.”

Tap Kibingwa pia ni sehemu ya dhamira pana ya Stanbic inapoadhimisha miaka 30 ya kutoa huduma nchini Tanzania. Kwa ujumbe elekezi “Tanzania ni nyumbani kwetu, na tunachochea ukuaji wake,” Benki ya Stanbic inaendelea kuwekeza katika huduma zinazoinua uzoefu wa wateja, kuleta ufikiaji, na kusaidia mabadiliko ya kiuchumi.

Benki inapoelekeza mwelekeo wake kwenye sura inayofuata ya uvumbuzi na ushirikishwaji wa wateja, ujumbe mmoja unaonekana wazi: dijitali sio siku zijazo—ni sasa hivi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *