Straika wa Kagera Sugar, Peter Lwasa, ameingia kwenye mnyukano wa usajili kati ya Mtibwa Sugar na Pamba Jiji FC.

Awali alikubaliana na Mtibwa, lakini Pamba imemshawishi kwa dau kubwa.
Hata hivyo, Kagera inasisitiza bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba na haiwezi kumuachia bure.
Lwasa alifunga mabao manane msimu uliopita na amewahi kucheza URA, KCCA (Uganda), Sofapaka, Gor Mahia (Kenya) na Lubumbashi Sports (DRC).


