Daraja la Mto Ruwembe lililopo Mikumi, linalounganisha Mji wa Mikumi na eneo la Ifakara, limekatika alfajiri ya leo baada ya kuharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwandishi wa habari aliyepo katika eneo la tukio ameshuhudia uharibifu huo wa daraja, ambao umesababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Mikumi na Ifakara. Barabara hiyo ni njia muhimu inayotumiwa na wakazi pamoja na wafanyabiashara katika ukanda huo kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Kwa sasa, vyombo vya uokoaji na usalama vimefika katika eneo la tukio na vinaendelea na jitihada za kuhakikisha usalama wa wananchi pamoja na watumiaji wa barabara hiyo.
Wakati huo huo, mamlaka husika zinatarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu chanzo cha uharibifu huo pamoja na hatua zinazochukuliwa kurejesha mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.




