Mwenda: Wachezaji wazawa tunalegalega

Beki wa kulia wa Yanga, Israel Mwenda, amesema tatizo kubwa kwa wachezaji wa Kitanzania ni kushindwa kudumisha viwango, wakilewa sifa na kupuuza mazoezi.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili, Mwenda alisema wengi hucheza vizuri kwa muda mfupi kisha kushuka kiwango kutokana na uvivu na kutokujitunza.

Amesema yeye binafsi amejiwekea malengo ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao, baada ya kuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA msimu uliopita.

“Nina deni kubwa kwa mashabiki. Siwezi kushuka kiwango msimu huu. Nataka niendelee kuwa bora,” alisema.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *