Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariMwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini, Frank Nyalusi afariki dunia

Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini, Frank Nyalusi afariki dunia

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini, Frank Nyalusi, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 19, 2025.

Nyalusi, ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Mivinjeni, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuanzia mwaka 2010 hadi 2020, alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Akizungumza na Maarifa Media leo, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), Necto Kitiga, amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu katika Mtaa wa Mawelewele, na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, John Heche, amesema chama kimepata pigo kubwa kufuatia kifo cha Nyalusi, akimtaja kama kiongozi jasiri, hodari na mwenye uzoefu mkubwa katika siasa za mageuzi.

“Kwa wale waliokaa kwenye siasa za mageuzi kwa muda mrefu wanajua — sio rahisi kumpata mtu kama Frank John Nyalusi kwa urahisi. Chama chetu kimepata pigo kubwa sana kwa kumpoteza mtu hodari, jasiri na mwenye uzoefu mkubwa,” ameandika Heche.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments