Saturday, March 7, 2026
spot_img
HomeHabariMwili wa mtu mmoja uonekana Jangwani, Dar

Mwili wa mtu mmoja uonekana Jangwani, Dar

Jangwani, Dar es Salaam – Mwili wa mtu mzima umeonekana asubuhi ya leo Agosti 27,2025 ukiwa unaelea kwenye mtaro karibu na kilipokuwa kituo cha mabasi ya mwendokasi, huku eneo hilo likiwa na ujenzi wa barabara mbadala kabla ya kubomolewa kwa barabara ya awali kwa ajili ya daraja la juu litakalounganisha Fire na Magomeni.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mabusi, amesema walipokea taarifa saa 3:30 asubuhi na timu ya uokoaji ilituma kufuatilia.

Amesema kuwa walikuta mwili wa marehemu Swalehe Shukurani chini ya daraja lenye maji na kuutoa saa nne kasoro asubuhi, kisha kukabidhiwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi katika Hospitali ya Polisi Barabara ya Kilwa.

Mabusi amesema mwili umetambuliwa na majirani waliotokea eneo la tukio, huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, akisema uchunguzi unaendelea na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments