Winga wa Azam FC, Idd Selmani ‘Nado’, amemkabidhi nahodha wa zamani wa timu hiyo, Himid Mao, jezi namba 23 aliyokuwa akiivaa, kama ishara ya heshima kwa mchango wake mkubwa ndani ya klabu hiyo.
Nado atatumia jezi namba 11 kuanzia msimu ujao na ameahidi msimu bora kwenye mashindano ya kimataifa.
Himid, ambaye aliwahi kuichezea Azam kati ya 2008–2018 kabla ya kwenda Misri, amerejea kujiunga na kikosi hicho kuelekea msimu mpya.
Wakati huo, Azam FC imewasili Juba, Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya El Merrikh Bentiu, Jumamosi ijayo.




