Wachezaji wa Namungo FC wamesema usajili wa wachezaji wapya katika dirisha dogo umeimarisha kikosi chao na kusaidia kuepuka kipigo katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Namungo imeshinda mechi mbili za ugenini na kutoka sare nyumbani, ikikusanya pointi 17 na kupanda hadi nafasi ya nane.
Nahodha Erasto Nyoni alisema wachezaji wapya wameleta nguvu mpya kikosini, na kuongeza kuwa wachezaji wa zamani wanawapa sapoti kubwa.
Wachezaji wapya ni kiungo Najib Mussa kutoka Singida Black Stars na mabeki Derrick Mukombozi na Emmanuel Charles.
Kocha Mkuu, Juma Mgunda, alisema ushindi dhidi ya Fountain Gate ilikuwa ni kisasi baada ya kupoteza mechi ya mzunguko wa kwanza.