Namungo FC imeweka rekodi ya kuachana na wachezaji 13 kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu, akiwemo Antony Mlingo aliyeuzwa Simba na Salehe Karabaka kurejea Yanga.

Wengine ni Beno Kalolanya, Emmanuel Asante, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Erick Malongi, Derick Mukombozi, Issa Abushehe, Joshua Ibrahim, Erick Kapaito, Emmanuel Charles na Anderson Solomon.
Klabu hiyo tayari imesajili Heritier Makambo na inatarajia kuimarika kama ilivyokuwa misimu ya nyuma.
Pamba Jiji FC nayo imeachana na wachezaji 11 akiwemo Christopher Oruchum, Deusa Kaseke na George Mpole, huku ikisajili Abdallah Idd Pina (mfungaji bora Zanzibar), Kelvin Nashon (kwa mkopo Singida Black Stars), Hassan Kibailo na Amos Kadikilo.


