
Mwezi Septemba 2024, NLD kilipokea wanachama 200 kutoka Tanzania Bara wakitoka ADC, na sasa chama hicho kimepokea zaidi ya wanachama 100 wilayani Handeni.
Katibu Mkuu wa Chama Cha NLD, Doyo Hassan Doyo akimkabidhi (kulia) akimkabidhi kadi ya chama hicho Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha ADC,Twaha Mngatwa, baada ya kujiunga na chama hicho.
Hatua hiyo inaonyesha kuimarika kwa chama hicho, huku chama hicho kikiongeza nguvu ya kisiasa na ushawishi katika maeneo mbalimbali nchini, hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
