Klabu ya Mashujaa FC imemtambulisha rasmi mshambuliaji Omari Omari aliyejiunga kwa mkopo kutoka Simba SC.

Omari amerudi katika klabu hiyo aliyotokea baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha Simba.
Mbali na Omari, Mashujaa pia imesajili straika Mudathir Said kutoka Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili, pamoja na Francis Magingi kutoka Geita Gold na Ismail Mgunda kutoka AS Vita ya DR Congo.
Klabu hiyo kutoka Kigoma imeanza rasmi kambi ya maandalizi kwa msimu ujao, huku wachezaji wakiendelea na mazoezi ya viungo kabla ya kuingia uwanjani. Mashujaa ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya saba kwa pointi 35, na sasa inalenga kufanya vizuri zaidi.