Onyango apigwa chini Dodoma Jiji – Munganga aingia

Beki wa Kenya, Joash Onyango, ametemwa na Dodoma Jiji FC pamoja na Hassan Mwaterema na Fadhil Mwinyimvua, klabu hiyo ikijiandaa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu na Kombe la FA.

Onyango aliyejiunga msimu uliopita kutoka Singida Black Stars, amewahi pia kucheza Simba na Gor Mahia ya Kenya. Dodoma Jiji imemsajili kiungo mkabaji kutoka DR Congo, Nelson Munganga (Tabora United), lakini imepoteza straika wake bora, Paul Peter, aliyejiunga na JKT Tanzania.

Wachezaji tisa wameongezewa mikataba kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *