Monday, April 6, 2026
spot_img
HomeHabariPolisi wathibitisha vifo saba wanaodaiwa kuiba nyeti

Polisi wathibitisha vifo saba wanaodaiwa kuiba nyeti

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwa watu saba wamefariki dunia, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa na kuendelea kupatiwa matibabu, baada ya kushambuliwa na wananchi waliowatuhumu kwa tuhuma za kuiba sehemu za siri—tukio linalochochewa na imani potofu zinazosambaa katika jamii.

‎Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa Aprili 5, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, matukio hayo yaliripotiwa Aprili 4, 2026 katika mikoa ya Dodoma, Rukwa, Songwe pamoja na Zanzibar, ambapo watu kadhaa walisingiziwa na kisha kushambuliwa kwa silaha za jadi.

‎Amesema hali hiyo imechangiwa na kusambaa kwa uzushi kuwa mtu anaweza kupoteza sehemu zake za siri kwa kuguswa begani, jambo ambalo si la kweli na halina msingi wa kisayansi.

‎Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza masikitiko yake kuona baadhi ya watu wakiendelea kushabikia na kusambaza taarifa hizo potofu kupitia mitandao ya kijamii, huku wengine wakizitumia kutengeneza maudhui ya vichekesho kwa lengo la kujipatia umaarufu au wafuasi (followers).

‎Polisi wamewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo vya dola wanapohisi kuwepo kwa tukio lolote la uhalifu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments