Polisi watoa pongezi kwa SGA kutimiza miaka 40 ya huduma bora

Jeshi la Polisi nchini limepongeza kazi nzuri zinazofanywa na kampuni za ulinzi binafsi ikiwemo kampuni ya SGA Security, ambapo limeahidi kushirikiana na kampuni hizo katika kuhakikisha usalama wa rai na mali zao.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa kitengo cha kampuni binafsi ya ulinzi makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (DCP) Ulrich Matei, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya SGA Security, iliyofanyika Dar es Salaam.

“Jeshi la polisi Tanzania, linaelewa umuhimu wa shughuli zinazofanywa na kampuni ya SGA Security, pia kama wadau wakubwa katika mawanda mazima ya ulinzi na usalama kutokana na kampuni hii kutumia mifumo bora katika maswala mazima ya ulinzi”, alisema na kuongeza, ni mifumo yenye kuzingatia taratibu na miongozo iliyotolewa na Jeshi la Polisi katika kibali kipya cha muongozo wa kampuni binafsi za ulinzi.

Aliendelea kusema kuwa kampuni ya SGA Security imewekeza vizuri kwenye mitambo ya kisasa, vitendea kazi vya uhakika, mafunzo kwa waajiriwa wao katika ngazi zote, mifumo mizuri ya utendaji, usimamizi thabiti, utayari wa ushirikiano na wadau wengi, ikiwemo serikalini huku ikizingatia matakwa ya kisheria na ya kijamii.

“Viwango vya utoaji huduma vya SGA Security ni vya kimataifa, na hii inadhirihishwa na tuzo nyingi ambazo wameshinda ikiwepo ISO certifications nne walizopata; ni mwanachama wa taasisi inayoshughulikia Kanuni za Kimataifa za Maadili ya Watoa Huduma za Usalama Binafsi (ICoCA), ikiwa ni mmoja ya makampuni chache zilizofikia kiwango hicho”, alisema na kongeza, mafanikio haya ni udhirihisho wa viwango vinavyotafutwa na wateja wengi, haswa kwenye sekta za kibalozi, madini, mafuta na gesi, kwa kuorodhesha machache.

DCP Matei ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camilius Wambura kwenye hafla hiyo, alisema kampuni ya SGA Security imeanza kukizingatia masuala ya mazingira, kijamii na utawala bora jambo ambali alisema linazingatia sana maswala hayo ikiwa ni sehemu ya kulinda mazingira na kuijiendeleza kwa njia endelevu.

Alizungumzia kampuni ya SGA Security kama mshindi mara mbili wa Tuzo ya milipa kodi mkubwa katika miaka ya 2021 na 2022, DCP Matei alisema hiyo ni heshima kubwa katika sekta ya ulinzi hususan kampuni binafsi.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa heshima hiyo mliyopata na pia ni ili kampuni yenu iendelee kuaminika na pia kushirikiana na serikali katika kutekeleza majukumu yenu”, alisema.

Aidha DCP Matei aliipongeza kampuni ya SGA Security kwa kuwajali wafanyakazi wake jambo ambalo alisema linadhihirishwa na zoezi la kuwazawadia pale muda wa kufanya hivyo unapwaadia.

“Tumesikia kwenye hotuba ya Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ambapo kuna mambo mengi sekta binafsi ya ulinzi inaweza kujifunza kutoka SGA Security; mfano mzuri ni ule wa kuwazawadia wafanyakazi; siyo kawaida kumpata mlinzi anayeifanyia kampuni moja kwa zaidi ya miaka 32; tumeambiwa pia kuwa wafanyakazi walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20 ni zaidi ya 600”, huu ni ushahidi ya kuwa huwa mnawajali wafanykazi wenu ndiyo maana wanaendelea kuwhapa kwa miaka mingi”, alisema.

DCP Matei aliipongeza kampuni hiyo kwa mpango wake wa mafunzo ya utayari wanaopewa walinzi kabla ya kuajiriwa sambamba na kuitikia wito wa jeshi la polisi linaloyataka makampuni binafsi ya ulizni kuajiri walinzi waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo).

“Ninayo Furaha kusikia ya kuwa SGA Security wanazingatia sana hili; pamoja na haya, nitoe rai kwenu kuhakikisha mnaajiri watu ambao hawana rekozi za aina yoyote ya uhalifu”, alisema.

“Tunaelewa wazi ya kuwa kabla ya kutoa ajira mpya, muongozo ulioko ni kuwa kampuni za ulinzi za binafsi ikiwemo SGA Security hutumia  utaratibu wa kuwapitisha katika mafunzo yanye malenga ya kuwaandaa waajiriwa wapya; mafunzo hayo hufanywa kwa kuzingatia muungozo wa Jeshi la Polisi na pia, tunashirikiana makampuni ya ulinzi kutoa mafunzo ya haki za kibinadamu”, alisema.

Aliongeza, “Napenda kuthibitisha kuwa SGA Security wamekuwa mstari wa mbele kwa kushirikisha Jeshi la polisi kabla ya kutoa ajira mpya, ambapo huwaandaa vijana wao kwa kazi; pamoja na mambo mengine, mimi nina imani kuwa hii ndio siri ya mafanikio ya kampuni ya SGA Security”.

“Nichukue fursa hii kuupongeza uongozi wa kampuni ya SGA Security kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa Jeshi la Polisi nchini katika azma yake ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao”, alisema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Security Bw Eric Sambu alisema kuwa, kampuni hiyo ambayo inatoa ajira zaidi ya 5,000 ilikuwa ni kampuni ya kwanza ya ulinzi binafsi kuanzishwa nchini.

“Kwa kuajiri Zaidi ya 5,000 hii inatafsiri wazi kuwa kampuni ya SGA Security inanufaisha zaidi ya watu 30,000 haswa ikizingatiwa kuwa mfanyakazi mmoja ana wategemezi sita (6)”, alibainisha.

Kwa mujibu Mkurugenzi Mkuu huyo, kwa kipindi cha miaka 40 ya kampuni hiyo, uongozi wake umekuwa ukizingatia vigezo vyote vya ubora vinavyohitajika katika kutoa huduma bora, jambo ambalo alisema limethibitishwa na tuzo mbalimbali za ubora ambazo kampuni hiyo imezipata katika kipindi chote cha uhai wake.

“Tuzo hizi ni pamoja na, ACOYA, Tuzo ya Maudhui ya Ndani, tuzo ya teknolojia bora ya Usalama wa Madini, Tuzo la Chaguo la Mlaji Afrika, Tuzo ya Ubora wa Afrika Mashariki na Tuzo ya Mlipa kodi Mkubwa”, aliongeza na kuongeza, uongozi wa kampuni hiyo unaendelea kufanya kazi kwa saa 24 katika kuhakikisha ukuaji endelevu wa taasisi hiyo.

Bw Sambu aliendela kusema kuwa, mafanikio makubwa ya kampuni hiyo yametokana na misingi mizuri ambayo alisema iliwekwa na waanzilishi wake aliotajwa kuwa ni Ed van Tongeren na Philemon Mgaya (wote marehemu) pamoja na juhudi kubwa za wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao alisema walifanya kazi kwa kujitolea, uaminifu, uthabiti na uvumbuzi.

“Kupitia wafanyakazi wetu waliojitolea tumetekeleza jukumu letu kama taasisi yenye ubora katika kutoa huduma; tumedhibiti uhalifu jambo ambalo limetoa fursa kwa wananchi kujikita katika kujenga taifa huku tukizingatia kwamba, usalama bora ndio jambo la muhimu kwa kila mtu”, alisema na kuongeza, mipango ya baadaye ya kampuni hiyo inaongozwa na mihimili minne ya taasisi hiyo aliyozitaja kuwa ni Ubunifu.

Mtazamo wa kisekta, utoaji wa huduma unaojumuisha Wote, na upanuzi wa huduma zake katika ngazi ya kikanda.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *