Klabu ya Tanzania Prisons, iliyoponea chupuchupu kushuka daraja msimu uliopita kupitia mechi ya mchujo, imetangaza kusajili wachezaji wapya wanne.

Hao ni Emmanuel Mtumbuka (Mashujaa FC), Abdallah Masoud ‘Cabaye’ (KenGold), Neva Kaboma (JKU) na Heritier Lulihoshi (Dodoma Jiji).
Wakati huohuo, Prisons imeachana na Beno Ngassa (sasa Dodoma Jiji) na Vedastus Mwihambi, huku ikiwapa mikataba mipya baadhi ya wachezaji waliopo.
Klabu hiyo kwa sasa ipo chini ya kocha mpya, Zedekiah Otieno kutoka Kenya, akichukua nafasi ya Amani Josiah.




