Mchungaji wa Kanisa la Embassy of God for All Nation, Isaac Paul Hammoud maarufu (IPM), amewataka waumini wa kanisa hilo na Watanzania kwa ujumla kuyapenda majeshi ya nchi na Serikali, kwa kuwa chuki dhidi ya mamlaka hizo ni kinyume na amri ya Mungu.
Ameijenga hoja yake hiyo, akirejea kitabu cha Kumbukumbu la Torati 8:10 inayosema, “utakula ushibe, utamshukuru bwana Mungu wako kwa nchi nzuri aliyokupa.”
Amesema ni bahati mbaya baadhi ya watu nchini kwa sasa, wanaona upendo kwa nchi na majeshi ni makosa, ilhali hakuna vyombo vingine vinavyoilinda nchi na wananchi zaidi ya hivyo.
“Hata kama kuna kitu wanakosea ni binadamu sio miungu wale. Tukubaliane kuna vitu vya kukubaliana tu. Lakini ni chuki, chuki, chuki, ukiiondoa Serikali kuna nchi tena hapo?,” amesema.












