PSSSF yaanza kwa kishindo michuano ya SHIMMUTA

Timu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF imenza kwa kishindo katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,(SHIMMUTA ) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Chuo cha Ardhi ya Jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo imeanza kutimua vumbi Jijini  Tanga kuanzia  Novemba 10 ambapo kikosi cha PSSSF kilianza kuonyesha makali yake kwa kuwachapa wababe wa Chuo hicho cha Ardhi.

Mashindano hayo yanayoshirikisha taasisi zaidi ya 91 nchini ni sehemu ya kuendeleza ujirani mwema, urafiki na ufanyaji wa mazoezi kwa wafanyakazi wa mashirika binafsi na ya umma lengo kuu likiwa ni kuendeleza na kukuza chachu ya michezo nchini.

Katika mashindano hayo, zaidi ya michezo 12 inashindaniwa, huku mpira wa miguu ukijizolea washiriki wengi zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *