Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo, Agosti 21, 2025, jijini Dodoma.

Kikao hicho kimeketishwa kwa ajili ya kufanya uteuzi wa Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.








