Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo februari 12, 2026 ameondoka nchini kuelekea Addis Ababa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika (AU), unaotarajiwa kufanyika Februari 14 hadi 15, 2026.









