Rais Samia akutana na viongozi wa TUCTA

Dar es Salaam, Agosti 12, 2025 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amekutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi wa TUCTA wamempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutekeleza ahadi yake ya kuongeza mishahara, kupandisha madaraja ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.

Viongozi hao wamesema hatua hizo zimeongeza ari na ufanisi wa watumishi wa umma, na kuonesha dhamira ya Serikali ya kusimamia haki na maslahi ya wafanyakazi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *