Wananchi wa Kibaigwa, wilayani Kongwa mkoani Dodoma, wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kujaza uwanja kwa maelfu ya watu waliokuwa na shauku ya kumsikiliza.

Wingi huo wa wananchi uliyopelekea shamrashamra kubwa, ulimfanya Dkt. Samia kushiriki furaha nao kwa kupiga picha ya pamoja kwa mtindo wa selfie, ikiwa ni kumbukumbu ya uungwaji mkono alioupata katika eneo hilo.
Mkutano huo umefanyika jioni ya leo ikiwa ni sehemu ya ratiba ya kampeni zake, ambapo Dkt. Samia amehitimisha ziara yake ya kampeni mkoani Morogoro na sasa anatarajiwa kuanza rasmi kampeni mkoani Dodoma.











