Januari 19 2025, Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, ulimchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Tumekusogezea namna Dkt Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho, alivyotoka nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, kutii kanuni ili kuupa uhuru Mkutano huo kufanya Uchaguzi.
