Rais Samia anawapenda wafungaji- Dk. Kijaji

✍🏿Takribani mifugo 4281 yachanjwa Arusha

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dk. Ashatu Kijaji amesema kuwa kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuidhinisha kiasi cha Bil. 216 kwa ajili ya ruzuku ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo kimedhihirisha mapenzi makubwa aliyonayo kwa wafugaji waliopo nchini.

Dk. Kijaji amesema hayo Julai 03, 2025 Wilayani Ngorongoro wakati akihitimisha ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa Mifugo katika mkoa wa Arusha ambapo takribani Mifugo 4281 imetambuliwa na kuchanjwa.

“Tayari Mhe. Dkt. Samia ameshatoa Bil. 65 zitakazotumika kwa ajili ya zoezi hilo kwa mwaka huu hivyo wafugaji tunaenda kunufaika na mifugo yetu kwa sababu tayari kuna soko linalohitaji tani Elfu 50 za nyama inayotokana na mifugo yetu iliyochanjwa na kutambuliwa” amesema Dk. Kijaji.

Aidha Dk. Kijaji amebainisha kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa miaka 5 wa uboreshaji sekta ya Mifugo ulioasisiwa na Mhe. Rais Samia katika kuhakikisha maisha ya wafugaji yanabadilika kupitia ufugaji wa kisasa unaoendana na matakwa ya soko la kimataifa.

Ziara hiyo ya Dk. Kijaji iliyolenga kukagua utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo iliyozinduliwa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Juni 16, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan itaendelea katika mikoa ya Mara, Simiyu, Geita, Pwani, Morogoro, Tabora na Dodoma.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *