MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Januari 2025, ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hiki ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliopangwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025, katika Jiji la Dodoma.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unatarajiwa kujadili na kupitisha masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya chama na mustakabali wa kisiasa nchini, huku ukihusisha viongozi wakuu na wajumbe kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.


