Rais Samia ateua viongozi 9 usiku huu

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi usiku huu leo Oktoba 30,2024 akiwemo Dk. Leonard Douglas Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Dk. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na anachukua nafasi ya Prof. Penina Mlama ambaye amemaliza muda wake.

Rais amemteua pia Prof. Zacharia Babubu Mganilwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Mganilwa ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na anachukua nafasi ya Dk. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake.

Mwingine ni Dk. Mwamini Madhebehi Tulli ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Dk. Tulli ameteuliwa kwa kipindi cha pili.

Rais amemteua pia Mhandisi Dk. Richard Joseph Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi Dk. Masika anachukua nafasi ya Prof. Henry Mahoo ambaye amemaliza muda wake.

Pia Balozi Salome Thaddaus Sijaona ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Balozi Sijaona ameteuliwa kwa kipindi cha pili.

Mwingine aliyeteuliwa ni Prof. Joseph Nicolao Otieno ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof Otieno ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na anachukua nafasi ya Prof. Hamisi Malebo ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samua amemteua pia Janet Reuben Lekashingo kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Lekashingo alikuwa Kamishna wa Tume ya Madini na anachukua nafasi ya Prof. Idris Kikula ambaye amemaliza muda wake.

Mwingine ni Asha Dachi Mbaruk ambaye ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Magazeti Tanzania (TSN), kabla ya uteuzi huu, Mbaruk alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Mwingine aliyeteuliwa na Rais Samia ni Mariam Salehe Mgaya ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji kwenye Rasilimali Madini, Mafuta na
Gesi Asilia (TEITI), kabla ya uteuzi huu, Mgaya alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *