Rais Samia aweka jiwe la msingi uzinduzi mradi wa maji Same – Mwanga – Korogwe

Rais Samia Suluhu Hassan, ameweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji Same – Mwanga – Korogwe wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Kilimanjaro leo, Machi 09, 2025.

Mradi huu ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa matumizi ya kila siku, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Kupitia mradi huu, wakazi wa maeneo husika watanufaika na upatikanaji wa maji wa uhakika, hali itakayopunguza changamoto za ukosefu wa maji na kuinua viwango vya afya na ustawi wa jamii.

Uzinduzi wa mradi huu unaashiria dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayolenga kuinua maisha ya Watanzania kwa vitendo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *