Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ataufufua Mkoa wa Morogoro kuwa wa viwanda.
Rais Dkt Samia ameyasema hayo mkoani Morogoro leo, Ijumaa Agosti 29, 2025 alipozungumza katika mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni za urais.
“Tunakuja kuifufua Morogoro kuwa Mkoa wa viwanda na hii kazi imeanza, kuna viwanda vilivyofufuliwa na kuna viwanda vipya vinavyokuja vikubwa na vidogo,” amesema.
Kwa mujibu wa Rais Dkt. Samia, tayari kazi hiyo imeanza kwa viwanda kufufuliwa, jitihada zitakazosaidia kuvutia uwekezaji na kuongeza fursa za ajira.
“Katika miaka mitano ijayo, tunakwenda kusimamia Morogoro irudi kuwa mkoa wa viwanda. Jitihada hizi zitatusaidia kuendeleza kuvutia uwekezaji na upanuzi wa viwanda katika mkoa wetu na hivyo kuongeza fursa za ajira,” amesema.




