Waziri wa Madini,Anthony Mavunde, amempokea Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, aliyewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika Februari 8, 2025.

Mkutano huu unalenga kujadili na kutafuta suluhisho kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.




